FMG Swahili Habari Siasa Michezo Udaku Mapenzi Biashara
Matangazo

Fei Toto Amfukuzia Aziz Ki Kwa Magoli, Atupia Moja

Fei Toto Amfukuzia Aziz Ki


Bao pekee la kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 13 limeipa klabu ya Azam FC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.


Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha alama 54 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa alama 4 na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.


Kwa upande wao Ihefu SC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na alama zao 25 za mechi 24 nafasi ya 11.


Powered by Blogger.