FMG Swahili Habari Siasa Michezo Udaku Mapenzi Biashara
Matangazo

PAUL Makonda aitwa kamati ya Maadili CCM

PAUL Makonda aitwa kamati ya Maadili CCM


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili na anatarajiwa kuitikia wito huo siku ya leo Jumatatu, Aprili 22, 2024.


Japo haijaelezwa anachoitiwa lakini inaweza kuhusishwa na kile Mkuu huyo wa Mkoa alichokisema wakati miaka 40 ya Kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa zamani Marehemu Edward Moringe Sokoine kuwa anawajua wale wanaotuma watu wamtukane mitandaoni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba miongoni mwao ni Mawaziri.


Kiongozi huyo wa Mkoa wa Arusha aliahidi kutaja orodha ya watu hao Jumatatu iliyopita lakini mpaka leo hajafanya hivyo.

Powered by Blogger.